
KARIBU TSA
Kuwawezesha wanachama wetu kijamii na kiuchumi kwa kuwapatia rasilimali na fursa zinazohitajika kusaidia kuboresha hali yao ya maisha.
MAONO YETU
Kujenga umoja thabiti unaowawezesha watanzania, na watu wengine wenye asili au nasaba ya kitanzania kusaidiana katika shida, raha na shughuli mbalimbali za kijamii. Kuwa mabingwa wa kuhamasisha na kusimamia utoaji wa misaada kwa mwanachama yeyote atakayepatikana na msiba wa kufiwa, ajali ya moto au chombo cha usafiri, kuugua kwa muda mrefu, na matatizo mengine yaliyoainishwa katika katiba.
​
Kujenga umoja na ushirikiano thabiti utakaowawezesha wanachama kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya fedha na uchumi, kufanya biashara za ndani na za kimataifa, na kuchangia kwa namna moja au nyingine katika kuinua kipato cha wanachama waliojiunga kuwekeza kwa mujibu wa katiba.
​
Kujenga ushirikiano utakaowawezesha wanachama kuwaleta pamoja watoto na wanafamilia wengine kwa lengo la kuwafundisha mila, desturi na tamaduni za kitanzania. TSA inaamini katika kukuza lugha ya kiswahili, kutunza mila na maadili ya kitanzania kwa faida ya vizazi vijavyo.
JUKUMU LETU
KUSAIDIANA KATIKA SHIDA NA RAHA MBALIMBALI ZA KIJAMII
Tanzania Sharing Association (TSA) inathamini uhai, furaha na ustawi wa kila mwanachama. Inapotokea mwanachama au mtoto wake kuaga dunia (kufariki) kikundi husaidia gharama za mazishi kwa kuchangia kiasi kinachofikia dola elfu kumi ($10,000). Kiasi hiki kinaweza kuongezeka au kupunguzwa kutegemea uhai wa mwanachama (status) na katiba ya TSA
TSA inaamini katika nguvu ya umoja katika kutatua matatizo ya watu. Mwanachama yeyote anapougua kiasi cha kushindwa kufanya majukumu yake ya kawaida, kufiwa na ndugu au mlezi, kuunguliwa moto au kupata ajali, TSA humpatia muhusika kiasi cha dola elfu tatu ($3,000) au elfu moja mia tano ($1,500) kutegemea hali ya muhusika na maelekezo ya katiba ya Tanzania Sharing Association.
UWEKEZAJI NA BIASHARA
TSA inathamini na kutilia mkazo mafanikio ya kiuchumi na kijamii ya kila mwanachama. Kwa sababu hiyo imeanzisha mfuko wa uwekezaji unaowawezesha wanakikundi wanaotaka kushirikiana katika biashara na uwekezaji. Mfuko huu unawahusu wanachama wa TSA tu.
MAKUZI YA WATOTO
TSA inavyo vikundi vidogo vidogo (clubs) vinavyo wakutanisha wanachama katika masuala mbalimbali ya kijamii. Mojawapo ya clubs hizo hushughulika na ustawi wa watoto wa wanachama. Club hii huandaa makongamano ya watoto, michezo na burudani
STAREHE NA BURUDANI
Tanzania Sharing Association inayo club maalum inayo shughulikia masuala ya starehe na burudani kwa wanachama wake. Club hii huandaa sherehe ya kuwapongeza wanachama kila mwisho wa mwaka, kwenye tarehe za katikati ya mwezi Desemba.
MAKUZI YA KIROHO
TSA haina dini wala haiko chini ya kikundi chochote cha kidini. Hata hivyo inathamini makuzi ya kiroho kwa wanachama wake. Kwa sababu hiyo wanachama hukutana kila mwisho wa mwezi kuomba pamoja na kutafakari maneno ya Mungu. Dini zote hushirikishwa.

VIONGOZI WETU
KAMATI YA UTENDAJI
Rose Lupiana
RAIS NA MKURUGENZI MTENDAJI
Tel: 1 206 602 0506
Faraja Mungai
KATIBU/MUHAKIKI
Tel: 1 206 602 0506
Irene Matanda
AFISA MAWASILIANO NA KIONGOZI WA VIJANA
Tel: 1 281 966 8284

WASILIANA
NASI
ANUANI YETU
Kwa mawasiliano ya haraka tafadhali jaza hii fomu:
RUDI JUU